26 Julai 2026 - 18:04
Ujenzi wa Masjid Imam Ali al-Naqi (as) Waendelea Katika Kijiji cha Kambozi Ikwiriri - Rafiki - Mkoani Pwani + Video na Picha

Ujenzi wa Masjid Imam Ali al-Naqi (as) unaendelea katika kijiji cha Kambozi Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani, Tanzania, chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Hujjatul Asr Foundation, Maulana Sayyid Arif Naqavi, katika jitihada za kuimarisha nyumba za ibada na huduma za kidini katika jamii.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, ujenzi wa Masjid Imam Ali al-Naqi (as) unaendelea katika kijiji cha Kambozi Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani, Tanzania.
 
Ujenzi wa Msikiti huo unasimamiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Hujjatul Asr Foundation, Maulana Sayyid Arif Naqavi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kujenga na kuimarisha miundombinu ya ibada na huduma za kidini kwa ajili ya Waislamu katika jamii.

Ujenzi wa Masjid Imam Ali al-Naqi (as) Waendelea Katika Kijiji cha Kambozi Ikwiriri - Rafiki - Mkoani Pwani + Video na Picha

Msikiti ni nyumba ya Mwenyezi Mungu na ni miongoni mwa maeneo matukufu yanayokusanya waumini kwa ajili ya kuswali, kumtaja Mwenyezi Mungu, kujifunza mafundisho ya dini na kuimarisha mshikamano wa kijamii.
 
Kwa msingi huo, kujenga msikiti ni miongoni mwa matendo yenye thawabu kubwa, kwani mtu anayeshiriki katika kujenga nyumba ya Mwenyezi Mungu anachangia kuendeleza ibada na kuandaa mazingira ya watu kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Ujenzi wa Masjid Imam Ali al-Naqi (as) Waendelea Katika Kijiji cha Kambozi Ikwiriri - Rafiki - Mkoani Pwani + Video na Picha

Mtume Muhammad (saw) amesema:
 
Mwenye kujenga Msikiti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamjengea nyumba Peponi.”
 
Ujenzi wa Masjid Imam Ali al-Naqi (as) unaendelea katika kijiji cha Kambozi Ikwiriri, huku ukitarajiwa kuwa kituo muhimu cha ibada, elimu ya dini na shughuli mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa eneo hilo baada ya kukamilika.

Ujenzi wa Masjid Imam Ali al-Naqi (as) Waendelea Katika Kijiji cha Kambozi Ikwiriri - Rafiki - Mkoani Pwani + Video na Picha

Maoni yako

You are replying to: .
captcha